• jingye group
  • jingye group
  • jingye group
  • jingye group
Maelezo ya Kampuni
Makazi yetu kwa sasa - Maelezo ya KampuniMaelezo ya Kampuni

Kampuni ya Jingye ipo katika jimbo la Pingshan mkabala na Xibaipo maarufu kama mji mtakatifu  wa ukombozi nchini China (Maka ya China). Katika kampuni hii tanzu ya Jingye shughuli ya utengenezaji wa chuma ndio biashara kuu japo imejikita katika shughuli nyingine mbadala za utengenezaji wa madawa, huduma za hoteli, ujenzi na ukodishaji wa majengo. Pia mpaka sasa imeajiri watu wapatao 20,500 na kumiliki rasilimali zenye thamani ya Yuan bilioni 22 na kuanzia mwaka 2011imelipa kodi ifikayo Yuan bilion 1.86. Mwaka 2013 kampuni ilithibisha mapato ya Yuan50.4 bilioni kwa mwaka na kushika nafasi ya 229 kati ya kampuni 500 kitaifa na namba tisa (9) kati ya 100 katika jimbo la Hebei vilevile inaongoza kati ya mashirika 100 katika jimbo la Shijiazhuang.

Jingye ni tegemeo kubwa duniani kwa utengenezaji wa chuma na bidhaa mbalimbali zenye viwango vya juu zitokanazo na chuma. Pia imethibitishwa kimataifa na kitaifa kwa ufanisi wake na kutunukiwa vyeti mbalimbali kama ISO 09001, ISO 14001 na CE cha Umoja wa Mataifa pamoja na ile ya kudumu ya utengenezaji wa chuma sahani imara zitumikazo katika utengenezaji wa  mitambo inayotumia mfumo wa mgandamizo wa mvuke. Vilevile kutokana na ubora bidhaa zake zimeshinda tuzo ijulikanayo kama kikombe cha dhahabu kutoka kwa jopo la Wataalamu wa Sayansi ya Utengenezaji na Matumizi bora ya Chuma ya nchini humo liitwalo China Iron and Steel Association. Hivyo basi ubora wa bidhaa zake umefanikisha kutumika katika miradi na kandarasi kama za ujenzi wa boti, sahani za kujengea madaraja, majengo marefu na miradi mbalimbali inayohitaji bidhaa za chuma zenye kuhimili matetemeko ya ardhi. Mafanikio katika mauzo ya bidhaa hizo nchini China na takribani nchi 30 na kanda tofauti katika mradi kama kama vile north-south water diversion, Maonesho ya kimataifa ya kibiashara China-Shanghai, njia mbadala ya Shijiazhuang na Ukumbi wa maonesho na burudani katika mji wa Taiyuan imekuwa ya mafanikio makubwa sana. Pia imepata heshima ya kutumia jina la jimbo la Hebei katika bidhaa zake na kupewa heshima kubwa ya usambazaji wa bidhaa zake iliyopewa heshima juu kwa usambazaji wa bidhaa zake na kampuni kama vile Shirika la Reli la Beijing la nchini China.

Vilevile Jingye Group inazingatia utunzaji wa mazingira hadi sasa imewekeza kiasi cha Yuan bilioni 2 hususani kuhimiza matumizi bora ya nishati, kupunguza uzalishaji wa hewa-ukaa. Pia inafuata kanuni na itikadi yake ya utunzaji wa mazingira usemao, “utunzaji wa mazingira usipokuwa na viwango na kutojali usalama wa wafanyakazi kampuni ifungwe”. Kufanikisha hilo kampuni imewekeza nguvu nyingi kuhakikisha mapinduzi ya kijani yanafanikiwa katika maeneo ya kiwandani na jimboni hapo kwa ujumla na kufikia 50% na kufanywa mfano katika shughuli za utalii jimboni Hebei.

Kwa mtazamo na malengo ya baadae Jingye Group pia imejikita katika utekelezaji wa mikakati ya maendeleo yake ya baadae inayolenga hasa uimarishaji, na uhamasishaji ili kuweza kutanua wigo wake katika uzalishaji na usambaziji ulio endelevu. Kutokana na mikakati hiyo Jingye imeweza kuongeza uzalishaji wa chuma kwa takribani tani milioni 12 kwa mwaka na kuongeza ubora wa bidhaa zake kwa kuweka mitambo ya kisasa ya kuchakata chuma na kuongeza tija katika utengenezaji na utoaji huduma yenye kuaminika ya usambazaji wa bidhaa. Katika uwekezaji Jingye Group imewekeza kwa kiasi kikubwa katika biashara zisizohusiana na uchumi utegemeao chuma, ujenzi na ukodishaji wa majumba ili kujiimarisha zaidi kimataifa. Kutokana na hivyo Jingye Group itafanikiwa kwa kufikia mapato yenye thamani ya Yuan bilioni 100 na hivyo kuwezesha uanzishwaji wa kampuni nyingine kubwa kama hii kwa miaka mitatu (3) ijayo.